Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka kufadhili utafiti kuhusu Zika

WHO yataka kufadhili utafiti kuhusu Zika

Shirika la Afya Duniani WHO linaorodesha tafiti zinazofanyika duniani kote kuhusu virusi vya Zika ili kubaini ni utafiti gani unaweza kusaidiwa ili kupata matokeo hima. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Taarifa iliyotolewa leo na WHO imeeleza kwamba kamati za wataalam zitatathmini tafiti hizo hivi karibuni.

WHO imesema kwa sasa hivi, kampuni 12 zinajaribu kubuni chanjo ya Zika, huku kampuni zingine zikijaribu kutengeneza dawa la kuzuia maambukizi jinsi ilivyokuwa kwa ugonjwa wa malaria.

Hatua hiyo ni miongoni mwa mradi uitwao R&D Blueprint ulioanza kutekelezwa na WHO baada ya mlipuko wa Ebola ili kuimarisha mfumo wa utafiti kuhusu maradhi ya kuambukiza.