Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio wakati wa majanga inasalia muokozi - UNESCO

Radio wakati wa majanga inasalia muokozi - UNESCO

Kuelekea siku ya Radio duniani tarehe 13 Februari mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limesema chombo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha jamii wakati wa majanga.

Katika ripoti yake yam waka 2015, shirikisho la msalaba mwekundu na hilal nyekundu limesema dunia imeendelea kukumbwa na majanga kama vile mafuriko, milipuko ya magonjwa, matetemeko ya ardhi na uchafu wa hali ya hewa ambapo Radio imedhirisha nguvu yake wakati wa majanga na hata baada ya majanga.

Imetolea mfano ripoti za kujikinga dhidi ya Ebola huko Liberia, Zika nchini Brazili na hata wakati wa Tsunami huko Japan na Chile na hivyo Irina Bokova Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO anatoa wito…

(Sauti ya Irina)

“Natoa wito kwa wanachama wa UNESCO kuunga mkono na kuimarisha uwezo wa radio ikiwemo zile za kijamii. Tunahitaji kuuimarisha ushirikiano kati ya watoa huduma za kibinadamu na wataalamu katika sekta ya radio.”

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema wakati wa majanga ya aina hiyo Radio inasalia chombo cha kurejesha uhai kupitia ripoti mbali mbali zinazowafikia watu wengi ili waweze kujikinga au kusaka maeneo salama.

Hata hivyo amesema wakati kama huo pia unaweza kuwa hatari kwa wanahabari ambao wanaweza kushindwa kupata habari hivyo ametaka siku ya radio duniani itumike kuangazia nafasi ya radio na jinsi ya kuimarisha majukumu yake.