Ban akaribisha muafaka ulioafikiwa Haiti:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa na wadau wote nchini Haiti ambayo yataruhusu kufanyika mipango ya mara moja ya kuendelea kufanya kazi kwa taasisi za nchi hiyo pamoja njia ya kuhitimika kwa utaratibu mchakato wa uchaguzi.
Akitambua kwamba muafaka huo upo ndani ya ari ya katiba ya nchi hiyo, Ban ametoa wito kwa pande zote husika kuutekeleza ili kuhakikisha kwamba madaraka yanahamishwa kwa njia ya kidemokrasia kwa maafisa waliochaguliwa.
Katibu Mkuu amewachagiza wadau wote kuendelea kushiriki katika majadiliano il kuongoza nchi yao katika mustakhbali imara na wa kidemokrasia ambao ni muhimu katika kushughulikia changamoto zinazowakabili.