Skip to main content

Baraza la Usalama kuchukua hatua muhimu dhidi ya DPRK :Power

Baraza la Usalama kuchukua hatua muhimu dhidi ya DPRK :Power

Hatua muhimu zitachukuliwa dhidi ya Jamhuri ya watu wa Korea yaani Korea ya Kaskazini DPRK, kufuatia kitendo chake cha kurusha kombora siku ya Jumamosi limesema baraza la Usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao maalumu cha baraza la Usalama Jumapili , balozi wa Marekani kwenye baraza la Usalama Samantha Power amesema kuna umuhimu wa zaidi ya uharaka kushughulikia hatua ya DPRK

“Tutakuja na hatua muhimu , tutakuja na hatua za kina. Tumejidhatiti kufanya jambo jipya. Tunategemea wajumbe wengine wa baraza ambao wanaona hili ni tishio kama tunavyoliona sisi, ili kujitokeza na kuungana nasi dhi ya lengo hili la pamoja”