Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limelaani vikali DPRK kurusha kombora jana:

Baraza la Usalama limelaani vikali DPRK kurusha kombora jana:

Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali urushaji wa kombora kwa kutumia teknolojia ya Balistik uliofanywa na Jamhuri ya watu wa Korea siku ya Jumamosi.

Kwenye kikao maalumu cha faragha cha baraza hilo siku ya Jumapili wajumbe wamesama tukio hilo nan a linguine lolote la DPRK liwe la angani au linachukuliwa kama la sateliti lianachangia katika katika hatua ya DPRK ya kutengeneza silaha za nyuklia na huo ni ukiukwaji mkubwa wa maazimio ya baraza la usalama namba 1718 (2006), 1874 (2009), 2087 (2013), na 2094 (2013).

Wamessisitiza kwamba tishio la wazi la amani na usalama wa kimataifa linaendelea hususani katika minajili ya majaribio ya nyuklia. Wajumbe wa baraza pia wameelezea nia yao ya kuanzisha hatua maalumu kwenye azimio jipya la baraza la usalama kwa ajili ya jaribio la nyuklia lililofanywa na DPRK hapo Jana January 6 ambapo DPRK imekiuka wajibu wake wa kimataifa .

Wajumbe wamekumbusha kwamba waliahidi kuchukua hatua zaidi endapo kutakuwa na tukio lingine la kurusha kombora litakalofanywa na DPRK. Wameongeza kuwa kwa maendeleo haya mapya baraza litapitisha azimio jipya litakalokuwa na hatua zaidi kukabiliana na hatari na ukiukwaji huo mkubwa.

Wajumbe wamesisitiza kuendelea kufanya kazi kuelekea suluhu ya amani, kidiplomasia na kisiasa katika hali hiyo ya DPRK katika jitihada za kutokomeza nuklia katika Ghuba ya Korea.