Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inasikitisha DPRK kurusha kombora kinyume na azimio la baraza la Usalama:Ban

Inasikitisha DPRK kurusha kombora kinyume na azimio la baraza la Usalama:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema inasikitisha sana kwa Jamhuri ya watu wa Korea DPRK kurusha kombora la kutumia teknolojia ya balistika na kukiuka azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la Februari 6 mwaka huu wa 2016 , licha ya wito kutoka jumuiya ya kimataifa ukipinga hatua hiyo.

Katibu Mkuu amerejea wito wake kwa DPRK akiitaka kusitisha vitendo vya uchokozi na kurudia kukubaliana na wajibu wake wa kimataifa.Amesisitiza utayari wake wa kushirikiana na pande zote kupunguza mvutano na kupata suluhua ya kauchana na nyuklia katika ghuba ya Korea.