Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yaonekana katika kutokomeza FGM Tanzania - Mtengeti

Nuru yaonekana katika kutokomeza FGM Tanzania - Mtengeti

Leo tarehe Sita Februari ni siku ya kutokomeza aina zote za ukeketaji watoto wa kike na wanawake. Umoja wa Mataifa ulifikia uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho pamoja na kukiuka haki za binadamu, kinakwamisha harakati za maendeleo ya kundi hilo wakati huu ambapo dunia inasaka siyo tu ulinzi wa kila binadamu bali pia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la idadi ya watu linashirikiana na wadau kutokomeza mila hiyo potofu. Miongoni mwa wadau ni Children's Dignity Forum ambao mimi Assumpta Massoi nilizungumza na mkurugenzi mtendaji wake Koshuma Mtengeti na hapa anaanza kwa kunieleza hadi sasa wamefanya nini.