Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao wa kuendeleza uhifadhi wa mazingira vyuoni wazinduliwa Kenya

Mtandao wa kuendeleza uhifadhi wa mazingira vyuoni wazinduliwa Kenya

Mtandao mpya umezinduliwa leo na Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, ukilenga kujumuisha vitendo vya kutunza mazingira na kukuza uendelevu katika mitaala na miradi ya utafiti ya vyuo vikuu nchini Kenya.

Zaidi ya washiriki 160 wamehudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa mtandao huo wa Kenya Green Universities Network jijini Nairobi, ambao ni mkakati wa pamoja wa Kamisheni ya Elimu ya Vyuo Vikuu nchini Kenya (CUE), Mamlaka ya Udhibiti wa Mazingira (NEMA), na Shirika la Mpango wa Mazingira (UNEP).

Mariam Osman ni afisa wa UNEP anayehusika na kuhamasisha wanafunzi wa chuo kikuu kuhusu kuhifadhi mazingira, na katika mahojiano na Grace Kaneiya wa idhaa hii, ameanza kwa kueleza umuhimu wa mkakati huo uliozinduliwa leo