Skip to main content

Fistula bado tatizo, UNFPA Tanzania wapania kuitokomeza

Fistula bado tatizo, UNFPA Tanzania wapania kuitokomeza

Fistula! Ugonjwa unaowakumba wanawake na wasichana kutokana na kuchelewa kupata huduma stahiki wakati wa kujifungua. Takwimu zinaonyesha kuwa licha ya mafanikio katika mbinu za kisasa za kutoa huduma ya afya bado takriban wanawake 800 wanafariki dunia kutokana na maradhi yatokanayo na uja uzito kila siku na kwa kila mwanamke anayefariki takriban wanawake 20 wanapata majeraha ya maisha kama vile fistula.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon akizungumzia janga hili la afya, anasema ni muhimu kupaza sauti ilikuchagiza maendeleo yatakayowezesha kumaliza ugonjwa wa Fistula. Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA ndilo lenye dhamana ya kuongoza harakati dhidi ya Fistula duniani ambapo nchini Tanzania, shirika hilo linashirkiana na serikali, taasisi binafsi katika kusongesha huduma hizo kwa kukabiliana na changamoto kadhaa ikiwamo huduma za afya za dharura na kupiga vita mila potofu kama vile ukeketaji au FGM ambayo nayo ni moja ya sababu ya Fistula.

Takwimu nchini humo zinaonyesha kuwa zaidi ya wanawake 2,000 kila mwaka hukumbwa na Fistula. Je jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu zinaonyesha matumaini?Na wanawake wenye Fistula wanasemaje? Tuungane na Stelius Sane wa redio washirika Wapo radio Fm ya jijini Dar es Salaam ambaye ametemblea moja ya hospitali zinazotoa tiba dhidi ya Fistula CCBRT.

(PACKAGE SANE)

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii, Mwakailishi Msaidizi wa UNFPA nchini Tanzania Dokta Rutasha Dadi anaeleza kile kinachofanywa na shirika hilo kutokomeza Fistula.

(MAHOJIANO)