Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya Lassa yatinga Benin, WHO, UNICEF zaikabili

Homa ya Lassa yatinga Benin, WHO, UNICEF zaikabili

Baada ya kugundulika kwa visa vinne vya homa mpya ya Lassa nchini Benin, serikali kwa kusaidiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na lile la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF), limeanza kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo.

Hadi sasa kuna visa dhaniwa 25 ambapo watu 12 wamefariki, kati ya vifo hivyo wanne kati yao wamethibitishwa kuathiriwa na Laasa. Wawili kati ya hao wanne wamefariki huku wengine wawili wanatibiwa katika karantini maalum.

WHO na UNICEF na wadau wengine wa masuala ya kibinadamu wameweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo ikiwamo karantini katika maeneo athirika, mifumo ya kufuatilia watu wanaohisiwa kuathiriwa, na kuweka wafanyakazi 200 ili kufuatilia visa pamoja na usambazaji wa dawa.

Homa ya Lassa husababaishwa na virusi vya Lassa na inaweza kusambazwa kwa binadamu kwa njia kadhaa, ikiwamo kupitia damu na mkojo. Homa hiyo imesharipotiwa nchini Liberia, Nigeria na Sierra Leone na inahisiwa kuwepo pia katika baadhi ya nchi za Magharibi.