Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wakimbizi 7,000 wawasili Italia na Ugiriki kwa siku nne: IOM

Zaidi ya wakimbizi 7,000 wawasili Italia na Ugiriki kwa siku nne: IOM

Idadi ya wahamiaji na wakimbizi wanaowasili nchini Italia na Ugiriki imefikia zaidi ya elfu saba hadi kufikia Februari nne limesema Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Katika chapisho lake IOM inasema kwamba katika siku nne za mwanzo wa mwezi, limeshuhudia kiasi hicho cha wahamiaji wakiwasili katika nchi hizo kiasi ambacho kimevuka kile cha Februari mwaka jana ambapo zaidi ya elfu sita walirikodiwa.

Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2016, IOM inakadiria kuwa zaidi ya wahamiaji 68,000 na wakimbizi wamewasili katika visiwa nchini Ugiriki.

Kati ya hao asilimia 44 ni wanaume, 22 wanawake na watoto wakiwa ni asilimia 34.