Julian Assange amewekwa kizuizini kiholela na Sweden na Uingereza:UM

Julian Assange amewekwa kizuizini kiholela na Sweden na Uingereza:UM

Mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange amewekwa kizuizini na Sweden na Uingereza tangu kukamatwa kwake mjini London tarehe 7 mwezi Desemba, 2010, kutokana na hatua za kisheria dhidi yake kutoka kwa serikali zote mbili, limesema jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya uwekwaji kizuizini kiholela. Flora Nducha na taarifa kamili..

(TAARIFA YA FLORA)

Watalaamu hao wametoa wito kwa serikali ya Sweden na Uingereza kumaliza hali ya kunyiwa uhuru kwa bwana Assange, na pia kumuwezesha haki yake ya kupipwa fidia. Sètondji Roland ADJOVI (pron. Seh-tond-ee Ho-loh Ad-joe-vee) ni mmoja wa wataalamu wa jopo hilo..

(SAUTI YA ADJOVI)

“Matokeo ya utafiti ni bayana na mapendekezo yamewekwa wazi kwa mataifa haya mawili husika,, Sweden na Uingereza kumaliza hali hii ya kizuizini kiholela. Haihusiani na jambo lingine lolote katika kesi yake kwa ujumla.”

Wataalamu hao wamesema nchi hizo mbili zimekiuka kifungu namaba 9 na 10 cha azimio la haki za binadamu kwa kumshikilia kwa muda wote huo Bwana Assange katika hali ya upweke bila kuwa na uhuru wa kutembea.