Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahofia hali ya wakimbizi na wahamiaji kwenye msitu wa Calais

UNHCR yahofia hali ya wakimbizi na wahamiaji kwenye msitu wa Calais

Takribani wakimbizi na wahamiaji 4000 wameripotiwa kuishi katika msitu wa Calais na wengine 2500 katika eneo la Grande- Synthe,pembezoni mwa Dunkerque,limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu hao wanaishi katika hali mbaya iliyochochewa zaidi na msimu huu wa baridi. UNHCR inahofia hususani hali ya watoto ambao wako peke yao na waliotenganishwa na wazazi au walezi wao.

UNHCR inataka hatua zichukuliwe hasa za kisheria ili kwa wale walio na ndugu zao kwenye muungano wa Ulaya waweza kujumuia nao haraka.