Skip to main content

Mtandao wa kukuza uendelevu vyuoni Kenya wazinduliwa na UNEP

Mtandao wa kukuza uendelevu vyuoni Kenya wazinduliwa na UNEP

Mtandao mpya umezinduliwa leo na Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, ukilenga kujumuisha vitendo vya kutunza mazingira na kukuza uendelevu katika mitaala na miradi ya utafiti ya vyuo vikuu nchini Kenya.

Zaidi ya washiriki 160 wamehudhuria kuzinduliwa kwa mtandao huo wa Green Universities Network, ambao ni mkakati wa pamoja wa Kamisheni ya Elimu ya Vyuo Vikuu nchini Kenya (CUE), Mamlaka ya Udhibiti wa Mazingira (NEMA), na Shirika la Mpango wa Mazingira (UNEP).

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, Achim Steiner, amesema kuwa Kenya inashuhudia hatua za kasi katika kuendeleza elimu ya juu, na kwamba kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa katika vyuo vikuu kunaongeza changamoto na fursa, na hivyo sababu zaidi ya kujumuisha tabia zilizo rafiki kwa mazingira na usambazaji wa maarifa katika mfumo wa elimu ya juu.

Mariam Osman ni afisa uhamasishaji wa UNEP nchini Kenya.

(Sauti ya Mariam)