Skip to main content

Vilabu vya wasichana vimejenga uwezo kukwepa ukeketaji

Vilabu vya wasichana vimejenga uwezo kukwepa ukeketaji

Wakati shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF likisema kuwa watoto na wanawake wapatao Milioni 200 katika nchi 30 wamekumbwa na ukeketaji, FGM nchini Tanzania harakati za kutokomeza mila hiyo potofu zimeanza kuzaa matunda.

Koshuma Mtengeti ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Children Dignity Forum nchini humo linaloendesha shughuli zake kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja kuanzisha vilabu vya wasichana..

(Sauti ya Koshuma)

Hata hivyo amesema changamoto ni pamoja makazi ya kudumu kwa wasichana waliokimbia mila ya ukeketaji akisema makazi ya sasa ni ya muda.

(Sauti ya Koshuma)