Bangura ataka manusura wa ukatili wa kingono wasaididhi we wanaposaka hifadhi

4 Februari 2016

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo, Zeinab Hawa Bangura, ametaka manusura wa ukatili wa kingono wapewe kipaumbele na kupatiwa huduma tosha zikiwamo za kimatibabu na kisaikolojia, wakati wa harakati za kusaka hifadhi.

Bi Bangura amesema hayo wakati wa kongamano la wahisani kuhusu Syria jijini London Uingereza, ambapo ameongeza kuwa wahanga na manusura wa ukatili wa kingono wanapaswa kuwekwa pamoja na familia zao, ili kuwapunguzia uchungu na pia kuhakikisha kuwa wanarejea katika maisha ya kawaida katika jamii haraka.

Aidha, ameongeza kuwa watoto wakimbizi wasioandamana na wazazi au walezi wanastahili kusajiliwa na kulindwa, ili wasije wakalengwa na wasafirishaji haramu katika biashara ya ngono na magenge mengine ya wahalifu.

Bi Bangura amesisitiza umuhimu wa nchi zinazowapa hifadhi wakimbizi kuwezesha upatikanaji wa haki, na kuwakabili wanaotekeleza uhalifu wa kingono kisheria.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter