Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yapokea dolamilioni 59 toka SDF

UNRWA yapokea dolamilioni 59 toka SDF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limepokea  msaada wa dola milioni 59 kutoka serikali ya Saudi Arabia kupitia shirika la mfuko wa maendeleo SDF, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi nchini Gaza, ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na Jordan

Taarifa ya UNRWA inasema kuwa mchango huo ulithibitishwa kupitia makubaliano yaliosainiwa mjini London mnamo Februari 14 na viongozi wa taasisi hizo yaani Kamishna Mkuu  wa UNRWA Pierre Krähenbühl na Makamu Rais wa SDF Mhandisi Yousef al-Bassam.

Serikali ya Saudi Arabia imeshachangisha kiasi cha dola milioni 500 hadi sasa kwa UNRWA na kufanya nchi hiyo kuwa ya tatu kwa kuchangia  katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

UNRWA imesema kuwa mchango huo pia umeifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa tume ya ushauri ambayo pamoja na kushauri pia humsaidia Kamishna Mkuu katika kutekeleza majukumu yake.