Skip to main content

Tanzania yaongeza maeneo ya kutoa huduma dhidi ya Saratani

Tanzania yaongeza maeneo ya kutoa huduma dhidi ya Saratani

Tanzania imeadhimisha siku ya saratani duniani kwa kuweka bayana tatizo la ugonjwa huo limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka ambapo takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini humo. Kiwango hicho ni sawa na asilimia 10 tu  kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani ‘Ocean Road’ ili kuweza kupata tiba.

Kama hiyo haitoshi kati ya hao wanaobahatika kufika kwa tiba, takribani asilimia 80 hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa ambazo ni hatua ya Tatu na ya Nne  hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo. Je hatua gani inachukuliwa? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Profesa Ayoub Magimba, Mkurugenzi msaidizi magonjwa yasiyoambukizwa katika Wizara ya Afya nchini humo ambapo anaeleza hatua zinazochukuliwa ikiwemo mkakati wa kitaifa dhidi ya Saratani wa mwaka 2013 hadi 2020, akianza kwa kuelezea unahusisha nini?