Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza mwelekeo wa uchaguzi ujao Somalia

UM wapongeza mwelekeo wa uchaguzi ujao Somalia

Akiwa ziarani nchini Somalia, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoaj wa mataifa kwa masuala ya kisiasa Jeffrey Feltman ameunga mkono jitihada za serikali ya Somalia katika kuendeleza utaratibu wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud bwana Feltman amesema kwamba uamuzi uliochukuliwa kuhusu uchaguzi umekuwa jasiri na sahihi.

Aidha ameipongeza serikali kwa kufikia mwafaka kuhusu mfumo wa uchaguzi.

(Sauti ya Bwana Feltman)

“ Umoja wa Mataifa umekaribisha ahadi ya kuwapatia wanawake asilimia 30 ya viti vya wawakilishi katika bunge la juu na la chini. Pia tunakaribisha ahadi ya kuendeleza mpango kazi wa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020 ili ifikapo mwaka 2020 kutakuwa na mfumo wa uchaguzi unategemea kura za watu na kukiri matarajio ya wasomali.”

Awali mwaka huu baraza la mawaziri limeamua kuunda mabunge mawili katika uchaguzi ujao.