Skip to main content

Ban na Mfalme Abdullah II wa Jordan wajadili mzozo wa Syria na wakimbizi

Ban na Mfalme Abdullah II wa Jordan wajadili mzozo wa Syria na wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan, pembezoni mwa kongamano la wahisani wa Syria jijini London, Uingereza.

Ban na Mfalme Adbullah wamezungumza kuhusu mzozo wa Syria, ambapo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu, Staffan de Mistura amempa taarifa mfalme huyo kuhusu mazungumzo kuhusu Syria, yaliyofanyika mjini Geneva hivi karibuni.

Ban amemshukuru Mfalme Abdullah na watu wa Jordan kwa mchango wao mkubwa kwa wakimbizi wa Syria waliokimbilia usalama wao nchini Jordan, akiongeza kuwa anadhamiria kuchagiza usaidizi kwa Jordan na nchi zingine kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati zinazowapa hifadhi mamilioni ya wakimbizi wa Syria.