Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kuanza kuwapatia watoto wa kike chanjo dhidi ya virusi vya HPV

Tanzania kuanza kuwapatia watoto wa kike chanjo dhidi ya virusi vya HPV

Wakati Shirika la Afya Duniani(WHO) likichagiza kinga dhidi ya saratani ambayo inazidi kusababisha vifo vya watu kila uchao, Tanzania imesema wakati wowote kuanzia sasa itaanza kuwapatia watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 13 chanjo dhidi ya virusi vya Human Papiloma, HPV vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi.

Mkurugenzi msaidizi magonjwa yasiyoambukizwa katika Wizara ya Afya nchini humo Profesa Ayoub Magimba ameiambia idhaa hii kuwa mpango huo umewezeshwa na ubia wa chanjo duniani, GAVI..

(Sauti ya Profesa Magimba)

Amesema hatua nyingine ni huduma ya matibabu kwa njia ya mionzi ya nyuklia ili kubaini na kutibu saratani itakayotolewa katika mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma..

(Sauti ya Profesa Magimba)

Nchini Tanzania idadi ya wagonjwa wapya wa saratani kila mwaka inakadiriwa kuwa Elfu 44 ambapo hata hivyo wanaoweza kufika hospitali kusaka huduma ni asilimia 10 pekee, wengi wao wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa huo.