Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ya DPRK kutaka kuzindua satilaiti inatatanisha:Ban

Hatua ya DPRK kutaka kuzindua satilaiti inatatanisha:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ameona taarifa kwamba Jamhuri ya watu wa Korea DPRK ikijumlisha mashirika kadhaa ya kimataifa kuhusu nia yake ya kutaka kuzindua satelaiti katika wiki zijazo.

Ban amesema maendeleo hayo ni hatua inayosumbua na itaongeza mashaka zaidi kwa jumuiya ya kimataifa ambayo tayari imetiwa hofu na jaribio la nyuklia la nchi hiyo hivi karibuni.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa DPRK kujizuia kutumia tekinolojia ya makombora ya balistika na badala yake kufanya kazi kwa ajili ya amani na utulivu kwenye rasi ya Korea.

Amesema yuko tayari kusaidia kupunguza mvutano na kuwezesha majadiliano na maridhiano.