Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC yaanza mkutano kumulika maendeleo kimataifa

ECOSOC yaanza mkutano kumulika maendeleo kimataifa

Tume ya maendeleo ya jamii ya Umoja wa Mataifa ECOSOC, leo imeanza mkutano wake wa 54 wa siku saba utakaojadili hali ya maendeleo kimataifa na changamoto katika kufikia melengo ya kukwamua jamii dhidi ya umasikini.

Katika hotuba yake kwa mkutano huo mkuu wa kitengo cha sera ya kijamii na maendeleo wa ECOSOC Bi Daniela Abas ambaye amewasilisha ripoti ya a Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema inaeleza umuhimu wa ujumuishwaji wa makundi na maeneo yote kwa ajili ya kusongesha ajenda ya maendeleo ya 2030 yaani SDGS.

Mathalani akizungumzia mabadiliko ya tabia nchi anasema

(SAUTI DANIELA)

"Katika zama hizi za kukuwa kwa ukosefu wa usawa, ukosefu wa usalama wa duniani uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na kuendelea kwa mzozo wa uchumi, chakula na nishati, pamoja na kuongezeka kwa matarajio ya ajira, sera thabiti za kijamii duniani ni muhimu. Ili kuongeza makabiliano na kutomuacha yeyote nyuma."

Mkutano huo uanatarajia kuwa na mijadala mbalimbali itakayokijikita katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ikiwamo kumulika maendeleo barani Afrika hususani kwa makundi maalum mathalani watu wenye ulemavu  na vijana.