Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wa Rwanda wasaidia kuimarisha ulinzi wa raia Malakal

Polisi wa Rwanda wasaidia kuimarisha ulinzi wa raia Malakal

Nchini Sudan Kusini, tangu mapigano yalipoanza miaka mitatu iliyopita, mji wa Malakal umeharibiwa na kutelekezwa. Maelfu ya wakazi wa mji huo na maeneo jirani walikimbilia kituo cha ulinzi wa raia cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS kutafuta usalama.

Kikiwa na mseto wa jamii zenye asili tofauti, zikiwemo makabila ya Dinka, Shilluk, Nuer na mengine madogomadogo, kituo hicho cha ulinzi wa raia hakijaweza kuepukana na mizozano ya kikabila na uhalifu. Kumulika hali ya usalama ilivyo, na doria inayowekwa na kikosi cha polisi wa Rwanda katika kituo hicho, ungana na Joshua Mmali katika Makala ifuatayo.