Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zote zihakikishe usalama kwa wanaopita uwanja wa vita Ukraine

Pande zote zihakikishe usalama kwa wanaopita uwanja wa vita Ukraine

Mashirika ya Misaada ya Kibinadamu nchini Ukarine yanahofia maelfu ya raia wanaokabiliwa na magumu kila siku wanapojaribu kuvuka eneo la machafuko. Mashirika hayo yanasema ni raia wa Ukraine ambao wengi wao ni wazee na wasiojiweza ambao wanapanga msitari kwa saa kadhaa kwenye baridi , ili kupata huduma ya dawa na chakula , kupata akiba zao za fedha za uzeeni na kuwaona ndugu zao.

Masharti pia yamewekwa kwa watu wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali karibu na eneo la mapambano. Wameongeza pia kufungwa hata kama ni kwa muda kwa kituo cha upekuzi kimoja au zaidi kutakuwa na athari kubwa kwa watu.

Timu ya Umoja wa Mataifa nchini humo kwa ushirikiano na mashirika hayo ya kibinadamu, wameitaka serikali kuacha wazi vituo hivyo vya upekuzi, amesisitiza mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Neal Walker, akiongeza kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa za pande zote katika mzozo zina wajibu wa kuhakikisha ulinzi kwa raia na kusaidia mashirika ya kibinadamu kupata fursa ya kuwafikia wahitaji.