Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kutokomeza FGM Tanzania imezaa matunda – UNFPA

Kampeni ya kutokomeza FGM Tanzania imezaa matunda – UNFPA

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa idadi ya watu, UNFPA limesema mpango wa miaka kumi wa harakati za kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, FGM nchini humo umekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko la wasichana wanaokimbia mila hiyo potofu ili kupatiwa mila mbadala.

Mwakilishi msadizi wa UNFPA nchini humo Christine Mwanukuzi-Kwayu ameiambia idhaa hii kuwa mila hiyo inahusisha sherehe na kupakwa poda badala ya kukeketwa na kwamba..

(Sauti ya Christine)

Na kama hiyo haitoshi wavulana nao wanasaidia dada zao katika kampeni hiyo akigusia kwenye kongamano moja ambapo..

(Sauti ya Christine)

Kwa mujibu wa mwakilishi msaidizi huyo wa UNFPA Tanzania, mikoa mitano ndiyo inaongoza ambayo ni Manyara, Dodoma, Singida, Arusha na Mara ambapo mkoani Manyara wanawake 81 kati ya kila 100 wamekeketwa.