Skip to main content

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la kigaidi la Damascus

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la kigaidi la Damascus

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi mjini Sayeda Zeinab kusini mwa viunga vya mji mkuu wa Syria Damascus lililotokea mwishoni mwa wiki.

Kundi la ISIL (Da’eesh) limekiri kuhusika na shambulio hilo lililokatili maisha ya watu Zaidi ya 60 na kujeruhi wengine wengi.

Wajumbe wa baraza wamerejea kuelezea wasiwasi wao kuhusu kundi la ISIL ikiwa ni pamoja na magaidi wapiganaji wa kigeni ambao wanajiunga na kundi hilo nchini Syria na makundi mengine ambayo yanahusiana na kundi la kigaidi la Al-qaida kuendelea na operesheni zao nchini Syria na kulaani athari za kuwepo kwao, itikadi kali, hali ya usalama na utulivu kwa Syria na nchi jirani.

Pia wametuma salamu za rambirambi kwa familia na jamaa wa walioathirika, na kwa serikali na waSyria wote kufuatia shambulio hilo.