Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwelekeo wa olimpiki Brazil na virusi vya Zika, WHO yazungumza

Mwelekeo wa olimpiki Brazil na virusi vya Zika, WHO yazungumza

Shirika la afya duniani, WHO limesema hadi sasa hakuna mwongozo wowote wa zuio la safari kwenda Brazil ambako virusi vya Zika vimeripotiwa na tayari virusi hivyo vimetangazwa kusababisha dharura ya afya ulimwenguni.

Mkurugenzi wa WHO anayehusika na afya ya mama, mtoto na vijiana barurabaru Dokta Antony Costello amesema hayo alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu mustakhbali wa michezo ya olimpiki ya majira ya kiangazi itakayofanyika nchini Brazil mwezi Agosti mwaka huu.

(Sauti ya Dokta Costello)

“Kwa sasa hakuna mapendekezo yoyote ya kamati ya dharura kuhusu zuio la biashara au safari. Ni wazi mtu kutoka nje ya ukanda huo mwenye wazo la kwenda huko akiwa mjamzito au ana mpango wa kupata ujauzito anaweza kufikiria uamuzi wake mwenyewe. Lakini hadi sasa hakuna mwongozo wowote.”