Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto na wanawake ndio idadi kubwa ya wanaokimbia:UNICEF

Watoto na wanawake ndio idadi kubwa ya wanaokimbia:UNICEF

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mtafaruku wa wakimbizi na wahamiaji Ulaya , kuna watoto na wanawake wengi Zaidi wanaokimbia kuliko wanaume, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Shirika hilo limesema watoto na wanawake sasa ni salimia 60 ya wakimbizi na wahamiaji wanaovuka mpaka kutoka Ugiriki kuingia Gevgelijia Jamhuri ya in Yugoslav ya zamani ya Macedonia. Na asilimia 36 kati ya hiyo wanatumia usafiri hatari wa boti kati ya Ugiriki na Uturuki.

Ingawa idadi kamili ya watoto wanaosafiri peke yao haijulikani , elfu 35,4000 wameomba hifadhi Sweden, wengi wakiwa kutoka Afghans, huku Ujerumani ikipokea barubaru 60,000 kutoka Syria, Afghanistan na Iraq.