Skip to main content

Dola milioni 354 zimeombwa kusaidia mahitaji ya kibinadamu Mali 2016:OCHA

Dola milioni 354 zimeombwa kusaidia mahitaji ya kibinadamu Mali 2016:OCHA

Mashirika ya kibinadamu nchini Mali yanasaka dola milioni 354 mwaka huu 2016 ili kusaidia watu walioathirika na vita nchini humo. John Kibego na taarifa kamili

(Taarifa ya Kibego)

Fedha hizo zinahitajika ili kutekeleza awamu ya tatu nay a mwisho ya mpango wa msaada wa kibinadamu ulioanzishwa na wadau wa masuala ya kibinadamu nchini Mali.

Jumla ya miradi 127 imepangwa kutekelezwa mwaka huu ili kusaidia watu milioni moja wengi kutoka maeneo ya Kaskazini na Katikati mwa nchi ambao wameathirika na vita.

Katika kuunga mkono mgono serikali ya Mali mpango huo wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa mataifa na yasiyo ya kiserikali NGO’s utashughulikia mahitaji ya muhimu, kuimarisha fursa ya mahitaji ya lazima kwa watu wasiojiweza, na kuboresha maisha yao.