Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazindua ombi la dola Milioni Tisa kukwamua Zika Brazil

UNICEF yazindua ombi la dola Milioni Tisa kukwamua Zika Brazil

Baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza kuwa virusi vya Zika ni dharura ya kimataifa, shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limezindua ombi la dola Milioni Tisa kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo hususan Amerika ya kusini ambako virusi vimeenea katika takribani nchi 25. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

UNICEF imesema huko Brazil, tayari inashirikiana na wadau na jamii kutuma ujumbe wa hamasa jinsi ya kuepuka kung’atwa na mbu na kutokomeza masalia ya wadudu hao na fedha hizo zitasaidia kupunguza makali ya madhara yake kwa watoto wachanga , familia na ukanda mzima wa Amerika ya Kusini.

Christophe Boulierac  ni msemaji wa UNICEF Geneva na amewaeleza waandishi wa habari kuwa...

(Sauti ya Christopher)

UNICEF imesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua haraka na kuwapatia wanawake na wajawazito taarifa sahihi wanazohitaji ili kujikinga wao na watoto wao na pia kushirisha jamii jinsi ya kudhibiti kuenea kwa mbu anayebeba virusi hivyo.”

Wakati huo huo WHO imesisitiza kuwa virusi vya Zika si tisho katika ujauzito kama HIV au Ebola lakini athari zake zina madhara makubwa sana kwa familia.