Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza rasmi

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza rasmi

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Syria na viongozi wa upinzani yameanza tena mjini Geneva, Uswisi, amesema leo Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura.

Amesema hayo baada ya kuzungumza na wawakilishi wa pande zote za mzozo, akiongeza kwamba anatarajia kuendelea na mazungumzo ya ana kwa ana na kila pande, lengo lake likiwa ni kuhakikisha mazungumzo yanaendelea.

Bwana de Mistura ameeleza msimamo wa wawakilishi wa chama cha upinzani kiitwacho HNC ambao wanataka, kabla ya kuanza mazungumzo na pande ya serikali, mashirika ya kibinadamu yapewe ruhusa ya kufikisha misaada ....

(Sauti ya de Mistura)

“Na wakati huo huo, wanasisitiza na sio wenyewe peke yao, kwamba wananchi wa Syria wakati tunajadili kuhusu mustakbali wa kisiasa wa nchi yao, wana haki ya kusikia na kushuhudia hali halisi kule waliko ikiwemo kupungua kwa ghasia, taarifa kuhusu mateka na maeneo ambayo bado yamezingirwa.”

Ameongeza kwamba kuna matumaini ya kuelewana kuhusu usitishwaji mapigano, akieleza kuwa raia wa Syria wanastahili kuona matokeo ya mazungumzo hayo.

hayo.