UNHCR Uganda kuendeleza harakati zake kusaidia wakimbizi
Uganda ni moja ya nchi ambayo inahifadhi wakimbizi kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Mmoja wa wafanaykazi wa Shirika hilo hivi karibuni amestaafu ambako kumefanyika hafla maalum ya kumuaga wakati akifungua ukurasa mpya katika maisha yake huku akipata anayechukua nafasi hiyo akiahidi kuendeleza majukumu ya UNHCR sanjari na ahadi kutoka serikalini.
John Kibego mwandishi wetu nchini Uganda alikuwa shuhuda basi ungana naye katika makala ifuatayo.