Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa Zika ni dharura ya afya ya kimataifa-WHO

Sasa Zika ni dharura ya afya ya kimataifa-WHO

Leo Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa virusi vya Zika ni dharura ya afya ya umma ya kimataifa.

Tangazo hilo limetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Margareth Chan baada ya mkutano wa wataalam uliofanyika mjini Geneva Uswisi kujadili mlipuko wa virusi vya Zika.

Bi Chan amewaambia waandishi wa habari kwamba uwezekano mkubwa wa uhusiano kati ya virusi hivyo na tatizo la watoto kuzaliwa na vichwa vidogo ni tukio lisilokawaida na linalohitaji jibu la kimataifa.

(Sauti ya Bi Chan)

« Wataalam wametilia maanani jinsi ugonjwa ulivyoenea hivi karibuni, kadhalika jinsi mbu wanaoweza kuambukiza ugonjwa huu walivyoenea duniani, ukosefu wa chanjo na vipimo vya mara moja, na ukosefu wa kinga mwilini kwa watu wanaoishi katika nchi zilizoambukiwa hivi karibuni, zote ni sababu za kutia wasiwasi zaidi. »

Dkt Chan ameongeza kwamba bado WHO haijapendekeza vikwazo vyovyote dhidi ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo, ila amesisitiza umuhimu wa kujikinga na mbu kwenye nchi hizo.