Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CHF yatoa dola milioni 9 kusaidia mahitaji ya kibinadamu CAR

CHF yatoa dola milioni 9 kusaidia mahitaji ya kibinadamu CAR

Mfuko wa kusaidia masuala ya kawaida ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, umezindua na kutenga dola milioni 9 kwa ajili ya msaada wa kuokoa maisha kwa watu waliotawanywa na mapigano, wanaorejea nyumbani, wakimbizi na jamii zinazowahifadhi.

Kwa mujibu wa mfuko huo CHF lengo la fedha hizo zilizotengwa ni kufadhili miradi ya kushughulikia mahitaji ya haraka ya kibinadamu ili kuimarisha hali ya watu walioathirika kwa kupata huduma muhimu na kuchangia kupunguza ghasia miongoni mwa jamii.

Ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuweza kukabiliana na mahitaji ya dharura ya kibinadamu nchini CAR, wahisani wamesaidia mfuko huo wa CHF ambao unawezesha wadau kupunguza machungu yanayowakabili mamilioni ya watu.

Mfuko huo unaosimamiwa na OCHA lengo lake ni kutoa ufadhili wa haraka wa fedha kwa ajili ya mahitaji muhimu ya kibinadamu ya dharura.