Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kutangaza majina ya wabakaji CAR

Umoja wa Mataifa kutangaza majina ya wabakaji CAR

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Raád Al Hussein amesema kwamba Umoja wa Mataifa unatarajia kutangaza majina ya nchi ambazo walinda amani wao wameshukiwa kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kingono. Ameongeza kwamba taarifa hizo zitatangazwa kupitia tovuti mpya itakayowezesha mtu yoyote kufuatilia harakati zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na suala hilo.

Kamishna Zeid amesema hayo leo akizungumza na  waandishi wa habari kwenye Umoja wa Mataifa, mjini Geneva, Uswisi, akikariri kwamba Umoja wa Mataifa unalaani vikali vitendo vyote vya uhalifu wa kingono, viwe vimetekelezwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa au na serikali binafsi.

Kuhusu ripoti za ubakaji unaodaiwa kutekelezwa na askari wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema mamlaka za serikali za Ufaransa zimeahidi kuchukua hatua zote zitakazohitajika kufualitia ripoti hizo.

Kuhusu walinda amani wa Umoja wa Mataifa akasema

(Sauti ya Kamishna Zeid)

“Umoja wa Mataifa umewahi kurudisha makwao kikosi vkzima, kwenye baadhi ya matukio. Na huenda utabidii kufanya hivyo tena, tukiendelea kushuhudia mfululizo wa ukiukaji huo, ambao utaonyesha kwamba nidhamu imeharibika kabisa kwenye baadhi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa.”