Kikao cha dharura chafanyika kujadili virusi vya Zika

Kikao cha dharura chafanyika kujadili virusi vya Zika

Huko Geneva, Uswisi shirika la afya duniani, WHO lina kikao cha kamati yake ya dharura kuhusu kanuni za afya za kimataifa, lengo likiwa ni kutathmini iwapo virusi vya Zika vinasababisha dharura ya kimataifa. Priscilla Lecomte na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Priscilla)

WHO iliitisha kikao hicho baada ya virusi hivyo kuendelea kuenea, sasa ikiwa ni katika mataifa 23, Brazil ikiwa imeathirika zaidi, ambapo kunadaiwa kuwepo kwa uhusiano kati ya virusi vya Zika na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo, Microcephaly.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan anasema wakati tafiti zinaendelea suala la msingi ni kinga kwa sababu..

(Sauti ya Dkt, Chan)

“Dimbwi dogo la maji linaweza kuwa mazalia ya mbu. Kwa hiyo kila mtu, familia na serikali zinaweza kuchukua hatua za pamoja za kinga ili kuzuia maambukizi.”