Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa vijana waanza makao makuu ya UM

Mkutano wa vijana waanza makao makuu ya UM

Mkutano wa Tano wa baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC kuhusu vijana unaanza leo kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Zaidi ya vijana 800 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanashiriki mkutano huo wa siku mbili ambapo maudhui ya mkutano ni nafasi ya vijana katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwezi Septemba mwaka jana.

Miongoni mwa yanayojadiliwa kwa kina ni nafasi na mchango wa vijana katika masuala ya afya, elimu, amani na ujumuishi katika jamii, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana, matatizo ya ajira na mabadiliko ya hali ya hewa.Jinsi gani vijana watasaidia kuyafanya ndoto hizi kuwa kweli.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, Ahmad Alhendawi amesema hii ni mara ya kwanza wanakutana tangu kupitishwa kwa SDGs na mwishoni wanatarajiwa kupitisha nyaraka muhimu ikiwemo..

(Sauti ya Alhendawi)

“Mpango wa kwanza wa kimataifa kuhusu ajira zenye hadhi kwa vijana ambao utawasilishwa katika kikao hiki cha pamoja cha vijana cha ECOSOC. Hii itakuwa ni habari njema kwa vijana kwamba zaidi ya mashirika 19 ya Umoja wa Mataifa yanakutana kuzindua mpango wa ajira zenye hadhi kwa vijana.”