Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Cyprus kushughulikia hali ya mahabusu

UM waitaka Cyprus kushughulikia hali ya mahabusu

Cyprus imeshuhudia maendeleo makubwa kuhusu jinsi watu wanavyotendewa mahabusu, lakini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi hususani kuhusiana na ufuatiliaji huru wa mahabusu na jinsi wanavyotendewa wahamiaji , imesema kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa juu ya kuzuia mateso (SPT) baada ya kutembelea nchi hiyo.

Kamati hiyo imesema imeridhishwa na hatu zilizopigwa baada ya kuzuru Cyprus lakini hali ya wale walioko katika vituo vya mahabusu za wahamiaji  inahitaji kuangaliwa kwa makini.

Ni muhimu sana kuhakikisha mahabusu hizo zinatumika tuu endapo ni lazima. Hali ya kizuizini ni lazima izingatie kwamba maeneo hayo sio magereza na wanaoshikiliwa humo sio wafungwa amesema Malcolm Evans,mwenyekiti wa kamati hiyo ndogo na mkuu wa msafara wa wajumbe wane waliokwenda Cyprus.

SPT kamati inayofuatilia jinsi mataifa yaliyotia saini mkataba wa kupinga unyanyasaji yanatimiza mwajibu wao ilikuwa Cyprus kuanzia Januari 25 hadi 29 na ilizuru pia vituo mbalimbali vya polisi, wodi ya wendawazimu na vituo vinavyohifadhi watoto na vijana wadogo wahamiaji walioingia nchini humo bila wazazi au walezi.