Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Syria : mjumbe wa Umoja wa Mataifa aendelea majadiliano

Mazungumzo ya Syria : mjumbe wa Umoja wa Mataifa aendelea majadiliano

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura anaendelea na majadiliano ya ana kwa ana na wawakilishi wa upinzani na serikali ya Syria, mjini Geneva, Uswisi.

Lengo la mazungumzo hayo yasiyokuwa rasmi ni kushawishi pande zote mbili zikubali kunzisha mazungumzo pamoja.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa Staffan de Mistura.

Bwana de Mistura ametembelea leo wawakilishi wa chama kimoja cha upinzani ambao waliwasili Geneva jumamosi usiku. Na Naibu wake Ramzy Ezzeldin Ramzy ametembelea wawakilishi wa serikali ili kuzungumzia jinsi mazungumzo ya amani yatakavyoendeshwa.