Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama latiwa mashaka na kuahirishwa duru ya mwisho ya uchaguzi Haiti

Baraza la usalama latiwa mashaka na kuahirishwa duru ya mwisho ya uchaguzi Haiti

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayoelekea kuahirishwa moja kwa moja duru ya mwisho ya uchaguzi nchini Haiti, ambao awali ulikuwa ufanyike Disemba 27, kisha ukaahirishwa kwa mara ya pili hadi Januari 24 na hadi sasa hauajafanyika.

Wajumbe wa baraza wamesema kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kunaweza kuathiri uwezo wa Haiti wa kushughulikia changamoto za kiusalama, kiuchumi, na kijamii zinazoghubika nchi hiyo na wamechagiza watendaji, bunge, na wadau wengine husika wa kisiasa kuja na makubaliano ifikapo Februari 7 mwaka huu utakaotoa muungozo kwa Wahaiti wa kuhitimisha mzunguko wa sasa wa uchaguzi na kuruhusu watu wa taiafa hilo kupata fursa ya kupiga kura kuchagua wawakilishi wao kwa uhuru, haki, ujumuishi na uwazi.

Baraza pia limepongeza mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSTAH na jeshi la polisi la Haiti kwa juhudi zao za kudhibiti ghasia na kuwalinda raia na kuongeza kuwa wataendelea kufuatilia kwa karibu hali kisiwani Haiti.