Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Paris kutoka COP21 umeanza kuzaa matunda:Pasztor

Mkataba wa Paris kutoka COP21 umeanza kuzaa matunda:Pasztor

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambaye amemaliza muda wake, Janos Pazstor, amesema mkataba wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka jana Paris, Ufaransa umeanza kuzaa matunda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Bwana Pasztor amesema dhihirisho hilo limetokana na ahadi zilizoanza kutekelezwa hata na sekta binafsi hususan katika nishati jadidifu au nishati mbadala.

Ametolea mfano taasisi ya Bloomberg ambayo wakati wa mkutano wa wawekezaji kwenye Umoja wa Mataifa ilitabiri mwelekeo wa matumizi ya nishati mbadala kwa mwaka huu wa 2016 ikihusisha mkataba wa Paris.

Bwana Pazstor amesema hiyo ni dalili njema na kama haitoshi..

(Sauti ya Pazstor)

“Na tunaona mwendelezo wa ahadi za  nishati mbadala na matumizi ya nishati bora licha kuporomoka kwa bei ya mafuta.”

Bwana Pazstor sasa ameteuliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mshauri wake mwandamizi kuhusu mabadiliko ya tabianchi.