Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya kusaka amani Syria yaanza Geneva

Mazungumzo ya kusaka amani Syria yaanza Geneva

Mazungumzo ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Syria yameanza leo mjini Geneva Uswisi,  licha ya kukosekana kwa uwakilishi wa upande wa upinzani.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ameanza kukutana na mwakilishiwa  kudumu wa serikali ya Syria katika Umoja wa Mataifa Bwana Bashar Jaafari.

Kiongozi  huyo anatarajiwa kuendelea kukutana na washiriki wengine wa mazungumzo wakiwamo wawakilishi wa asasi za kiraia.

Mazungumzo hayo yameelezwa na mwakilishi wa UM kwa Syria kuwa ya karibu ambapo pande shiriki zitakutana na kiongozi huyo kwa nyakati tofauti.