Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watu walazimika kuhama makwao Mashariki mwa DRC, MONUSCO yaongeza ushirikiano na FARDC

Maelfu ya watu walazimika kuhama makwao Mashariki mwa DRC, MONUSCO yaongeza ushirikiano na FARDC

Mashambulizi yanayofanyika na waasi wa Mai-Mai, FDLR, na ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamelazimisha maelfu ya watu kukimbia makwao,

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo limesihi mamlaka za serikali kukabiliana na hali ya kiusalama na kuwapatia makazi wakimbizi hao wa ndani.

Leo Dobbs ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva Uswisi

(Sauti ya bwana Dobbs)

“ Hii inatia wasiwasi sana, ghasia inayoendelea nchini DRC ni habari inayosahaulika sana. Haipewi uzito unaostahili . Tunadhani ni wakati sasa kuweka silaha chini na kugeukia utulivu’’

Wakati huo huo msemaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, Felix Bass amethibitisha leo kwamba vikosi vya usalama vya MONUSCO kwa kushirikiana na jeshi la kitaifa FARDC wameongeza idadi ya askari wao mpakani wa Burundi kwenye eneo la Uvira, Kivu Kaskazini kutokana vitisho vya usalama kutoka Burundi.

Bwana Bass ameongeza kwamba FARDC na MONUSCO siku ya alhamis wamesaini makubaliano ya kurejesha ushirikiano wao nchini DRC.