Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Burundi kila pande inavutia kwake: Balozi Delattre

Hali ya Burundi kila pande inavutia kwake: Balozi Delattre

Leo Baraza la Usalama limejadili kuhusu ziara yake nchini Burundi, huku  Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Francois Delattre akikariri maombi ya Baraza hilo kwa mamlaka za serikali ya Burundi. Taarifa zaidi ya Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Balozi Delattre amewasilisha ripoti ya ziara hiyo ambayo iliandaliwa na ujumbe wa Ufaransa na Angola wiki iliyopita.

Amesema wawakilishi wote wa vyombo vya habari na asasi za kiraia wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu usalama wao na haki zao, huku wawakilishi wa serikali na Rais Pierre Nkurunziza wakidai hali ni nzuri na ripoti za waandishi wa habari ni uongo.

Kuhusu habari zilizotolewa leo za kufungwa kwa mwandishi wa habari wa Ufaransa na mpigaji picha akasema

(Sauti ya Balozi Delattre)

" Ufaransa inaziomba mamlaka za serikali ziwachilie huru mara moja, huku harakati za kidiplomasia zikiendelea kwa minajili hiyo."