Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inawezekana kuondoa mafuta ya kisukuku: Kyte

Inawezekana kuondoa mafuta ya kisukuku: Kyte

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nishati endelevu kwa wote Rachel Kyte amesema inawezekana kutimiza  lengo la kuondoa mafuata yatokanayo na kisukuku na  kuongeza maradufu uwekezaji katika nishati safi ifikapo mwaka 2020.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa, Bi Kyte amesema lengo hilo lililowekwa na Katibu Mkuu linawezekana akisisitiza muhimu ni.

(SAUTI KYTE)

‘Tutoweshe uchafu katika mfumo kwanza, tuongeze garama kwa hewa ukaa na hiyo itatoa ishara kwa wawekezaji kuwekeza katika nishati safi kisha tutapata dola bilioni 329 kwa mwka ambazo zitakuwa zimewekezwa katika nishati safi tayari.’’

Amesema kwa kutekeleza hili hakuna atakayeachwa nyuma na kuwezesha kila mmoja kupata maji safi na nishati rahisi.