Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya Gbagbo si kesi dhidi ya Cote d’Ivoire- ICC

Kesi ya Gbagbo si kesi dhidi ya Cote d’Ivoire- ICC

Mjini The Hague Uholanzi kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na Laurent Gbagbo na mshirika wake Charles Ble Goude imeanza leo rasmi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Jaji Cuno Tarfusser wa Italia anayeongoza kesi hiyo akisema si kesi dhidi ya Cote d’Ivoire.

(Sauti ya Jaji Tarfusser)

« Hii ni kesi ya jinai, siyo maandamano ya kisaisa, wala mchezo ambapo pande moja inataka kushinda nyingine. Siyo kesi dhidi ya Cote d’Ivoire kabisa, wala dhidi ya raia wa Cote d’Ivoire, lakini dhidi ya watu wawili walioshtakiwa na uhalifu na mwendesha mashtaka. »

Jaji Tarfusser ameongeza kwamba kesi itaendeshwa na uwazi, usawa na kwa kufuatilia sheria tu, na kwamba hataruhusu kesi hiyo itumiwe katika maswala ya kisiasa.

Jaji Tarfusser akamhoji kila mshtakiwa iwapo anakubali au anakana mashtaka....

Nats...

Anasema Bwana Laurent Gbagbo unakiri au unakana..

Gbagbo akasema...

Nats...

Nakana mashtaka dhidi yangu..

Bwana Charles Ble Goudé naye alikana mashtaka yote dhidi yake ambapo awali aliulizwa na Jaji Tarfusser

Nats..

Anamwuliza unaelewa msingi wa mashtaka dhidi yako . Ndipo Bwana Goudé akajibu.

Nats...

Ndio naelewa msingi wa mashataka dhidi yangu.

Laurent Gbagbo ambaye alikuwa rais wa Cote d’Ivoire ameshtakiwa na uhalifu wa kibinadamu, mateso, mauaji na ubakaji, vitendo ambavyo vinadaiwa kutekelezwa na vikosi vya usalama vya Cote d’Ivoire na vikundi vya vijana baada ya uchaguzi wa rais wa Cote d’Ivoire wa mwaka 2010. Kwa upande wake Charles Ble Goude ambaye ameshtakiwa na uhalifu huo huo alikuwa waziri wa vijana na ajira kwenye serikali ya Gbagbo.