Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa chakula wazidi Yemen- FAO

Uhaba wa chakula wazidi Yemen- FAO

Zaidi ya watu milioni 14 wanakumbwa na ukosefu wa chakula nchini Yemen, limesema leo Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO, likisema ni ongezeko la asimilia 36 ikilinganishwa na mwaka 2014.

FAO katika taarifa imesema uhaba wa chakula umesababishwa na mapigano na mfumuko wa bei za bidhaa zinazoingizwa kutoka nje,  ambazo zinachangia asilimia 90 ya vyakula vya raia.

Naibu Mwakilishi wa FAO nchini Yemen Etienne Peterschmitt amesema FAO imetoa ombi la dola milioni 25 kwa mwaka 2016 ili kuimarisha uwezo wa wayemen wa kujitegemea:

(Sauti ya bwana Peterschmitt)

“Bila shaka ni kulenga sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.  Namaanisha kwamba  tutajaribu kuimarisha uchumi wa kilimo, kushughulikia matumizi ya maji, kwa sababu maji ni swala la msingi. Tukifanikiwa kutekeleza hayo yote, tutakuwa tumefikia watu wapatao 700,000.”