Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwelekeo wa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania watia matumaini- UNFPA

Mwelekeo wa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania watia matumaini- UNFPA

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango imeonyesha ongezeko katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania. Takwimu zinasema kuwa matumizi sasa ni asilimia 27 ya watanzania wenye uwezo wa kutumia njia hizo ikiwemo sindano, vipandikizi na mipira ya kiume na ya kike.

Lakini ni hatua gani ambazo zimechangia ongezeko hilo japo linaelezwa kuwa ni la wastani? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Felister Bwana, Afisa programu wa afya ya mama na mtoto kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu, UNFPA nchini humo.

Kwanza anaanza kwa kuelezea changamoto ambazo wamekumbana nazo katika kufanikisha mpango huo ikiwemo fikra potofu za matumizi ya njia za uzazi wa mpango.