Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya Ebola, Sierra Leone yapiga hatua kukuza haki za binadamu

Licha ya Ebola, Sierra Leone yapiga hatua kukuza haki za binadamu

Leo hali ya Sierra Leone ikifanyiwa tathmini ya haki za binadamu kwenye kikao cha Baraza la Haki za Binadamu huko Geneva Uswisi, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Joseph Fitzerald Kamara amesema kwamba mlipuko wa Ebola ulisimamisha kwa muda jitihada za serikali katika kukuza maendeleo na haki za binadamu nchini humo.

Ameeleza kwamba rais alilazimika kutangaza hali ya dharura iliyopiga marufuku shughuli za kijamii na maandamano yote.

Hata hivyo, waziri huyo amesema hali hiyo imeondolewa sasa na Sierra Leone inaendelea kuendeleza harakati zinazotunza haki za watoto, wanawake, vyombo vya habari na demokrasia kwa ujumla.

Ametaja mfano wa ukeketaji ambao ni mila ya utamaduni nchi humo akisema

(Sauti ya Waziri Kamara)

“ Sierra Leone imeshirikiana na viongozi wa jamii ili kuelimisha watu kuhusu madhara ya mila hiyo na kuwapatia vyanzo mbadala vya kipato kupitia mikopo midogomidogo. Serikali imepitisha sheria inayokataza unyago kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18.”